DRC-CENI-JOSEPH KABILA

UN: Baraza la Usalama limekutana kujadili uchaguzi wa DRC

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakikutana kujadili hali ya mambo nchini DRC. 21 October 2013
Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakikutana kujadili hali ya mambo nchini DRC. 21 October 2013 UN Photo/Paulo Filgueiras

Baraza la usalama la umoja wa Mataifa, hapo jana limekutana katika kikao cha faragha kujadili uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wakati huu mataifa yenye nguvu yakisubiri kutangazwa kwa matokeo.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu uliombwa kufanyika na nchi ya Ufaransa wakati huu umoja wa Ulaya na umoja wa Afrika wakizitaka mamlaka nchini humo kuheshimu matokeo ya uchaguzi uliofanyikan Desemba 30.

 

Matokeo ya awali yalitarajiwa kuanza kutangaza siku ya jumapili lakini tume ya uchaguzi CENI juma hili ilijitokeza na kueleza uwezekano wa kuchelewa kutangazwa kwa matokeo hayo.

 

Katika hatua nyingine umoja wa Mataifa umeonya kuhusu kuendelea kukamatwa kwa wanasiasa na raia kutoka katika vituo vya kuhesabia kura, umoja huo ukisema vitendo vya ukamataji havikubaliki na unafuatilia kwa karibu yanayojiri.

 

Matokeo ya uchaguzi wa Jumapili iliyopita yataamua ni nani atamrithi rais Joseph Kabila aliyekaa madarakani kwa karibu miaka 18.