SUDAN-MAANDAMANO-BASHIR-SIASA

Maandamano zaidi yaitishwa nchini Sudan

Waandamanaji nchini Sudan
Waandamanaji nchini Sudan REUTERS

Wanaharakati nchini Sudan wamehimiza maandamano zaidi dhidi ya rais Omar Al Bashir, kumshinikiza aondoke madarakani.

Matangazo ya kibiashara

Wito huu umekuja, muda mfupi baada ya kumfuta kazi Waziri wake wa afya kwa sababu ya kupanda kwa gharama ya kupata matibabu nchini humo.

Maandamano dhidi ya rais Bashir, kumtaka ajiuzulu, yamekuwa yakiendelea tangu mwezi Desemba mwaka 2018, baada ya kupanda kwa bei kwa gharama ya mkate.

Watu 19 wakiwemo maafisa wawili wa usalama wameuawa katika maandamano hayo ambayo yameshuhudia makabiliano makali kati ya waandamanaji na maafisa wa usalama.

Rais Bashir, anayashtumu mataifa ya nje kwa kwa kuchochea maandamano hayo ambayo yanashuhudiwa nzima, licha ya kuunda kamati maalum ya kuangazia chanzo cha maandamano hayo.