DRC-SIASA-UCHAGUZI-KURA

Tume ya Uchaguzi nchini DRC yahairisha kutangaza matokeo ya urais

Corneille Nangaa Yobeluo,Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini DRC
Corneille Nangaa Yobeluo,Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini DRC AFP/Luis Tato

Tume ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imeahirisha hadi wiki ijayo kutangaza matokeo ya awali ya Uchaguzi wa urais, baada ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu mwisho wa mwaka 2018.

Matangazo ya kibiashara

Raia wa DRC walikuwa wamesubiri kutolewa kwa matokeo hayo, hivi leo kwa mujibu wa ratiba iliyokuwa imetangazwa hapo awali na Tume ya Uchaguzi.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Corneille Nangaa amesema siku ya Jumapili, haitawezekana kutangaza matokeo hayo kwa sababu mchakato huo bado haujapatikana.

Tume ya Uchaguzi haijatangaza tarehe ya kutolewa kwa matokeo hayo wakati huu, wananchi wakisubiri matokeo hayo kwa hamu licha ya kuwepo kwa hali ya wasiwasi.

Ushindani mkali unashuhudiwa kuwa kati ya mgombea wa chama tawala Emmanuel Ramazani Shadary, Martin Fayulu na Felix Tshisekedi wote kutoka upande wa upinzani.