DRC-UFARANSA-SIASA-TSHISEKEDI

Ufaransa yasema Martin Fayulu alionekana kushinda Uchaguzi

Rais wa Ufaransa  Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron REUTERS/Benoit Tessier/Pool

Ufaransa imesema matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi nchini humo, na kumpa ushindi Felix Tshisekedi, sio ya kuaminika.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya nje Jean-Yves Le Drian amesema, kwa namna matokeo yalvyokuwa yanatangazwa, Martin Fayulu alistahili kushinda.

“Inaonekana wazi kuwa, matokeo yaliyotangazwa hayaendani na sio matokeo sahihi,” amekimabia kituo cha Habari cha Ufaransa Cnews.

Aidha, ameongeza kuwa kwa namna matokeo yalivyokuwa, Bwana Fayulu alikuwa anaongoza katika Uchaguzi huo.

“Bwana Fayulu, alionekana mshindi wa Uchaguzi huu,” aliongeza.

Fayulu aliyekuwa anawakilisha muungano wa Lamuka, amesema matokeo yaliyotangazwa, sio ya kweli.

Matokeo hayasio ya kweli, haoneshi ukweli uliokuwepo kwenye sanduku la kura,” ameiambia Radio France International.

Mahakama ya Katiba ina wiki moja kuthibitisha matokeo hayo kabla ya rais mpya hajaapishwa.