NIGERIA-UCHAGUZI-SIASA

Muhammadu Buhari: Nina imani kuwa nitashinda uchaguzi

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari. Reuters

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amesema ana uhakika wa kushinda muhula wa pili, wakati wa Uchaguzi Mkuu unaopangwa kufanyika mwezi Februari mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 76, ameendelea na kampeni nchini humo kuelekea uchaguzi huo utakaofanyika tarehe 16 mwezi Februari.

Wagombea 73 wanawania urais, lakini ushindani unatarajiwa kuwa kati ya Buhari na mgombea wa chama kikuu cha upinzani PDP Atiku Abubakar.

Buhari mwenye umri wa miaka 75, anawania muhula wa pili wa miaka minne, kuongoza taifa hilo la Afrika Magharibi lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika, huku ujumbe wake wa kampeni ukiwa ni kuendeleza vita dhidi ya ufisadi.

Hivi karibuni Rais huyo aliwaambia wafuasi wake jijini Abuja, kuwa kwa muda wa miaka minne ambayo amekuwa madarakani, ametekeleza ahadi ya kuimarisha usalama lakini pia kupambana na rushwa.

Buhari anapambana na aliyekuwa Makamu wa rais Atiku Abubakar, anayepeperusha bendera ya chama kikuu cha upinzani cha PDP, huku wachambuzi wa siasa wakisema ushindani utakuwa ni mkali.

Wagombe 78 kutoka vyama 91, wanawania urais nchini Nigeria.