SUDAN-MAANDAMANO-UCHUMI

Omar al-Bashir: Utawala wangu hautoachia ngazi kwa maandamano

Rais wa Sudan Omar al-Bashir.
Rais wa Sudan Omar al-Bashir. AFP/ Desmond Kwande

Rais wa Sudan Omar al-Bashir amesema leo Jumatatu kuwa maandamano ambayo yanaendelea kuikumba Sudan kwa karibu mwezi mmoja hayatatoondoa utawala wake wa karibu miongo mitatu.

Matangazo ya kibiashara

Ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara wa wafuasi wake katika mji wa Darfur, magharibi mwa Sudan.

"Maandamano haya tasababisha mabadiliko ya utawala," amesema Bashirmbele ya umati wa wafuasi wake katika huko Niyala, mji mkuu wa Darfur, kufuatia kutokea kwa maandamano ya kwanza jana Jumapili ya kupinga serikali katika mkoa ulioshuhudia vita vya umwagaji damu tangu mapema mwaka 2000.

"Kuna njia moja tu kwa utawala, na njia hiyo ni uchaguzi. Wananchi wa Sudan watapiga kura mnamo mwaka 2020 kuamua rais wao mpya," amesema Bashir, mwenye umri wa miaka 75, ambaye anatarajiwa kuwania kwa muhula wa tatu mwaka ujao.

Maandamano ya sasa nchini Sudan yalianza tarehe 19 Desemba mwaka 2019 kufuatia uamuzi wa serikali ya kuongeza mara tatu bei ya mkate.