COTE D'IVOIRE-ICC-HAKI

Hatima ya Laurent Gbagbo kujulikana Jumanne hii baada ya uamuzi wa ICC

Laurent Gbagbo, Hague tarehe 5 Desemba 2011.
Laurent Gbagbo, Hague tarehe 5 Desemba 2011. REUTERS/Peter Dejong/Pool

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC inatarajia kutoa uamuzi wake Jumanne wiki hii kuhusu kumuachilia huru au la rais wa zamani wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo.

Matangazo ya kibiashara

Laurent Gbagbo na waziri wake wa zamani Charles Blé Goudé, pia kiongozi wa zamani wa vuguvugu la vijana wa chama tawala wakati huo wanashtumiwa uhalifu dhidi wa binadamu katika vurugu zilizozuka kati ya mwezi Desemba 2010 na Aprili 2011, kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais.

Kesi yao ilianza Januari 28, 2016.

Tangu kuanza kwa kesi hiyo, mwendesha mashitaka amewaita mashahidi 82. Kwa upande wa Eric MacDonald, msaidizi wa mwendesha mashitaka, amesema Laurent Gbagbo na Charles Blé Goudé ni sehemu ya "kundi dogo maalumu" lililoanzisha "mpango wa pamoja" ili kusalia madarakani kwa njia zote zinazohitajika, ikiwa ni pamoja na matumizi ya vurugu dhidi ya raia ambao watakuwa hawawaungi mkono. "Bw Gbagbo alihimiza majeshi ambayo yalikuwa tiifu kwake kufanya uhalifu. Agosti 27, 2010, katika mji wa Divo, aliwaambia wasithubutu kuacha kutekeleza maagizo aliyowapa, alisema Eric MacDonald, mwezi Oktoba mwaka uliyopita. Aliwaambia kuwa hakuna mtu atakayehukumiwa kwa makosa yake. Aidha, Laurent Gbagbo hakuchukua hatua za kuzuia uhalifu kutokea wakati wa mgogoro, " amebaini Bw MacDonald.

Mwezi Novemba mwaka jana, upande wa utetezi uliomba kuachiliwa huru. Wanasheria wa Laurent Gbagbo wanabaini kwamba mwendesha mashitaka ameshindwa kuthibitisha kuwepo kwa "mpango wa pamoja", anaweka mbele, kama ushahidi usioaminika. Upande wa utetezi unatilia shaka ushahidi uliokusanywa na mwendesha mashitaka wakati wa uchunguzi wake. “Na hiyo ndiyo sababu halisi ya kuwa sheria hazijafuatiwa, “ Bw MacDonald ameongeza