ZIMBABWE-MAANDAMANO-UCHUMI

Watu wengi wauawa katika maandamano Zimbabwe

Wafuasi wa chama cha upinzani cha MDC, nchini Zimbabwe, wakipinga hali ya kiuchumi na utawala wa Rais Emmerson Mnangagwa.
Wafuasi wa chama cha upinzani cha MDC, nchini Zimbabwe, wakipinga hali ya kiuchumi na utawala wa Rais Emmerson Mnangagwa. © Jekesai NJIKIZANA / AFP

Watu wengi wameuawa siku ya Jumatatu nchini Zimbabwe wakati wa maandamano yaliyogubikwa na vurugu dhidi ya kupanda kwa kasi kwa bei ya mafuta iliyotangazwa na Rais Emmerson Mnangagwa.

Matangazo ya kibiashara

Zimbabwe ni nchi ambayo inakabiliwa na mgogoro wa kijamii kutokana na mgogoro wa kiuchumi na kifedha.

Siku ya kwanza ya mgomo mkuu wa siku tatu, polisi waliingilia kati katika miji miwili mikubwa ya nchi hiyo, Harare na Bulawayo (kusini), kwa kutawanya mamia ya watu wenye hasira ambao walizuia barabara na kupora madukani. kuzorotesha shughuli mbalimbali.

Operesheni hiyo "ilisababisha maafa makubwa na mali nyingi kupotea, pamoja na watu waliojeruhiwa kati ya polisi na raia," Waziri wa Usalama Owen Ncube amesema Jumatatu jioni, bila kueleza idadi ya watu waliopteza maisha au kujeruhiwa.

"Tunatoa rambi rambi zetu kwa familia zilizopoteza ndugu zao," ameongeza, bila maelezo zaidi.

Muungamo wa vyama vya wafanyakazi nchini humo umeitisha pia mgomo wa siku tatu, kupinga nyongeza hiyo. Rais Emmerson Mnangangwa Jumamosi iliyopita, alitangaza kupanda kwa bei ya mafuta kwa asilimia 100 kutokana na uhaba wa bidhaa hiyo muhimu.