COTE D'IVOIRE-ICC-HAKI

ICC yamuachilia huru Laurent Gbagbo na Charles Blé Goudé

Rais wa zamani wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, Hague Januari 15, 2019.
Rais wa zamani wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, Hague Januari 15, 2019. Peter Dejong/Pool via REUTERS

Majaji wamefutilia mbali ombi la mwendesha mashitaka kuendelea kumzuia rais wa zamani wa Cote d'Ivoire na waziri wake wa zamani Charles Ble Goude.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu umekuja siku moja baada ya ICC kumfutia mashataka Gbagbo na msaidizi wake Charles Ble Goude na kuamuru waachiliwe huru, uamuzi ambao ulifuatiwa na rufaa ya waendesha mashitaka dhidi ya uamuzi huu wa majaji.

Tangazo lilitolewa muda mfupi kabla ya saa 10 alaasiri, saa za Hague, na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Majaji wameomba maafisa wa ICC kuhakikisha kurudi kwa wawili hao kwenye makao makuu ya Mahakama ikiwa itahitajika.

Uamuzi huu ulikuwa ukijadiliwa na Mahakama tangu Jumatano asubuhi. Kwa upande wa waendesha mashitaka, kulikuwa na "sababu za kipekee" kupinga kuachiliwa huru kwa wawili hao. Waendesha mashitaka wana wasiwasi kwamba Laurent Gbagbo na Charles Blé Goudé watakataa kuripoti mbele ya Mahakama ikiwa kesi hiyo itasikilizwa katika kitengo cha rufaa.

Majaji wa Mahakama wa ICC, wakiongozwa na Jaji Cuno Tarfusser walimwachilia huru Gbagbo na msaidizi wake  Goude baada ya kubainika kuwa upande wa mashataka haukuwa na ushahidi dhidi yao.Wakati wa machafuko nchini Cote d'Ivoire, watu zaidi ya 3,000 walipoteza maisha katika machafuko hayo.