DRC-AU-UCHAGUZI-SIASA

Kagame aitisha kikao cha mazungumzo cha Umoja wa Afrika kuhusu DRC

Paul Kagame, Rais wa Rwanda na pia Rais wa sasa wa Umoja wa Afrika (AU), akitoa hotuba kwenye Makao makuu ya Umoja wa Afrika Addis Ababa, Ethiopia, Novemba 17, 2018.
Paul Kagame, Rais wa Rwanda na pia Rais wa sasa wa Umoja wa Afrika (AU), akitoa hotuba kwenye Makao makuu ya Umoja wa Afrika Addis Ababa, Ethiopia, Novemba 17, 2018. © AFP

Viongozi nchi za Umoja wa Afrika wanatarajia kukutana Alhamisi wiki hii mjini Addis Ababa, nchini Ethiopia kwa ajili ya mkutano wa "ngazi ya juu" kuhusu hali nchini DRC, taarifa kutoka Umoja wa Afrika imesema.

Matangazo ya kibiashara

"Rais wa Rwanda pia Rais wa Umoja wa Afrika (AU) Paul Kagame anatarajia kuitisha mkutano wa mazungumzo wa ngazi ya juu utakao washirikisha viongozi 16 wa nchi za Afrika kuhusu hali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, "taarifa hiyo imebaini.

Mkutano huo utatanguliwa na mazungumzo ya ndani ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Nchi ya DRC inakabiliwa na mgogoro wa baada ya uchaguzi.

Martin Fayulu, mmoja wa wapinzani wakuu walioshindwa katika uchaguzi wa urais wa Desemba 30, 2018, ameendelea kupinga matokeo ya awali ya uchaguzi yanayompa ushindi Felix Tshisekedi Tshilombo, kiongozi wa chama cha upinzani cha UDPS, ambaye alishinda kwa 38.57% ya kura.

Mahakama ya Katiba inaendelea kusikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais iliyofunguliwa na Martin Fayulu.

Matokeo hayo pia yanapingwa na mgombea mwingine, Theodore Ngoyi, ambayae anataka uchaguzi huo ufutwe mara moja.