IVORY COAST-GBAGBO-SIASA

Kiongozi wa mashtaka ataka Laurent Gbagbo asirejee nchini Ivory Coast

Rais wa zamani wa Ivory Coast  Laurent Gbagbo
Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo Peter Dejong/Pool via REUTERS

Viongozi wa mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC, wamewataka Majaji kumzuia rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo kurejea katika nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Ombi hili limekuja siku moja baada ya Majaji wa Mahakama hiyo, kumfutia mashataka Gbagbo na msaidizi wake Charles Ble Goude na kuamuru waachiliwe huru.

Majaji wanakutana siku ya Jumatano kujadili masharti ya kumwachilia Gbagbo, ambaye anatarajiwa kuondoka mjini Hague wakati wowote.

Gbagbo alikamatwa na kufikishwa katika Mahakama hiyo ya Kimataifa mwaka 2011, baada ya mzozo wa kisiasa nchini mwake kati yake na raia wa sasa Allasane Ouattara.

Majaji wa Mahakama hiyo, wakiongozwa na Jaji Cuno Tarfusser walimwachilia huru Gbagbo na msaidizi wake  Goude baada ya kubainika kuwa upande wa mashataka haukuwa na ushahidi dhidi yao.

Wakati wa machafuko hayo, watu zaidi ya 3,000 walipoteza maisha katika machafuko hayo.