COTE D'IVOIRE-ICC-HAKI

Mwendesha mashitaka akata rufaa dhidi ya uamuzi wa kuachiliwa huru Gbagbo na Ble Goude

Rais wa zamani wa Cote d'Ivoire ataendelea kusubiri ili kuona kama ataachiliwa huru au la.
Rais wa zamani wa Cote d'Ivoire ataendelea kusubiri ili kuona kama ataachiliwa huru au la. © Peter Dejong/Pool via REUTERS

Rais wa zamani wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo na waziri wake wa zamani Charles Ble Goude huenda wakaendelea kusalia kwa muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa katika jela la Scheveningen.

Matangazo ya kibiashara

Jumatano jioni Mwendesha mashitaka wa ICC Fatou Bensouda alikata rufaa dhidi ya uamuzi wa kuachiliwa huru siku moja baada ya ICC kumfutia mashataka Gbagbo na msaidizi wake Charles Ble Goude na kuamuru waachiliwe huru.

Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa (ICC), Fatou Bensouda, ameomba Laurent Gbagbo na Charles Ble Goude kuendelea kuzuiliwa jela, wakati anaendelea kupata na kutathmini sababu zilizopelekea majaji kuamua kuachiliwa huru.

Fatou Bensouda ana hofu kwamba rais wa zamani wa Cote d'Ivoire na waziri wake wa zamani wanaweza kutoroka kabla ya kuendelea kwa kesi dhidi yao.

Alhamisi wiki hii majaji watano wa Mahakama ya Rufaa wanatarajia kuamua kama wanakubali au la rufaa ya mwendesha mashtaka iliyowasilishwa Jumatano jioni. Kama ombi la mwendesha mashitaka litakubaliwa Laurent Gbagbo na Charles Ble Goude wataendelea kuzuiliwa katika kituo jela la Scheveningen.

Kwa upande mwingine, ikiwa majaji watano watakataa rufaa na kuthibitisha uamuzi wa mahakama wa kuwafutia mashitaka, hatua itakayofauata ni kuachiliwa huru bila masharti.

Tayari nchi ya Ubelgiji imekubali kumpokea Laurent Gbagbo kama ataachiliwa huru.