NIGERIA-UCHAGUZI-SIASA

Obasanjo : Buhari ana mpango wa kuiba kura

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari. Reuters

Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo amemshtumu rais wa nchi hiyo Muhammadu Buhari, anaye wania kiti cha urais kwa muhula wa pili, kwamba anaandaa mpango mkubwa wa kuiba kura ili aweze kushinda Uchaguzi Mkuu wa Februari 16.

Matangazo ya kibiashara

Bw Obasanjo, ambaye alimuunga mkono Rais wa sasa wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015, katika miezi ya hivi karibuni ameendelea kukosoa sera yake, na wakati huu anamuunga mkono mgombea mkuu wa upinzani katka uchaguzi wa urais, Atiku Abubakar .

"Binafsi, nina mashaka makubwa kuhusu uadilifu, uhuru wa INEC (Tume ya Uchaguzi) kwa kuandaa uchaguzi wa haki, ulio huru na wa kuaminika," amesema Obasanjo katika barua iliyowekwa wazi.

Pia amemshtumu moja kwa moja Rais Buhari, kuwakwamba amenaz kuajiri maafisa ili kuchakachua matokeo ya uchaguzi kabla ya uchaguzi.

"Watu wake wanafanya kazi usiku na mchana na maafisa wa usalama pamoja na maafisa uchaguzi ili kukamilisha mpango wao kwa kuhesabu matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa, uchaguzi wa magavana wa mikoa na uchaguzi wa urais kwa kumpa ushindi, " amesema Obasanjo

Bw Obasanjo amemfananidha Rais Buhari na dikteta wa zamani wa nchi hiyo Sani Abacha, ambaye alitawala Nigeria tangu mwaka 1993 hadi 1998, akisema kuwa alikuwa tayari kufanya kilio chini ya ueezo wake ili asalie madarakani.