ZIMBABWE-MAANDAMANO-UCHUMI

Rais Mnangagwa asitisha ziara yake nje ya nchi

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa. REUTERS/Philimon Bulawayo

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ametangaza kuwa anasitisha ziara yake nje ya nchi baada ya maandamano na ukandamizaji wa kikatili nchini mwake, akisema anataka "Zimbabwe yenye utulivu, na amani".

Matangazo ya kibiashara

"Kutokana na hali ya kiuchumi, ninarudi nyumbani baada ya wiki moja mazungumzo chanya kuhusu biashara ," Mnangagwa ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter,akisem anasitisha ushiriki wake katika mkutano wa Davos unaoanza leo Jumatatu. Zimbabwe itawakilishwa katika mkutano huo na Waziri wa Fedha Mthuli Ncube.

Mnangagwa, ambaye amekuwa kitafuta wawekezaji wa kigeni, siku ya Jumapili alifanya ziara ziara nchini Kazakhstan, baada ya kuanza ziara yake siku ya Jumatatu nchini Urusi.

Watu wasiopungua 12 waliuawa na wengine 78 walijeruhiwa kwa risasi wiki iliyopita, kwa mujibu wa Shirikisho la mashirika yasiyo ya kiserikali ya Haki za Binadamu nchini Zimbabwe, shirikisho ambalo liliorodhesha kesi zaidi ya 240 za ukatili na mateso.

Lakini ukandamizaji huu wa kikatili ni "kihonjo," ameonya msemaji wa rais George Charamba, akinukuliwa siku ya Jumapili na gazeti la serikali la The Sunday News, akishtumu upinzani kuchochea vurugu.

Charamba anaambatana na rais katika ziara yake nje ya nchi.