DRC-SIASA-USALAMA

DRC yaendelea na maandalizi ya kutawazwa kwa rais mpya

Rais Mteule wa DRC Felix Tshisekedi Tshilombo.
Rais Mteule wa DRC Felix Tshisekedi Tshilombo. AFP

Rais mteule wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi Tshilombo, aliyetarajiwa kuapishwa Jumanne wiki hii, sasa anatarajiwa kula kiapo siku ya Alhamisi Januari 24, 2019.

Matangazo ya kibiashara

Hii imethibitishwa na Lydie Omanga, msemaji wa muungano wa upinzani ulioshinda uchaguzi huu, kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi, baada ya kuzungumza na Shirika la Habari la Ufaransa AFP.

Muungano wa CASH ulioshinda uchaguzi huu unasema tukio hili la kihistoria, ambalo litanyika baadaye wiki hii, limeahirishwa ili kumalizia maandalizi ya kukabidhi madaraka kwa amani katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati.

Hata hivyo kwa mujibu wa chanzo kilio karibu na utawala wa Kinshasa, zoezi hilo limeahirishwa kwa sababu za kifedha.

Felix Tshisekedi alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa Desemba 30 mwaka jana lakini mgombea mwengine wa upinzani martin fayulu ameendelea kupinga ushindi huo na kubaini kwamba yeye ndio aliyeshinda uchaguzi kwa 60% ya kura.