DRC-SIASA

Rais mpya DRC kuapishwa Alhamisi

Félix Tshisekedi akitia saini kwenye mkataba uliofikiwa chini ya usuluhisho wa Maaskofu kanisa Katoloki Kinshasa, Desemba 31, 2016.
Félix Tshisekedi akitia saini kwenye mkataba uliofikiwa chini ya usuluhisho wa Maaskofu kanisa Katoloki Kinshasa, Desemba 31, 2016. REUTERS

Kuna uwezekano kuwa rais Mteule wa DRC Felix Tshisekedi huenda akatawazwa Alhamisi wiki hii kwenye makao makuu ya Bunge la nchi hiyo, vyanzo vilio karibu na ofisi ya rais vimebaini.

Matangazo ya kibiashara

"Sherehe za kutawazwa kwa rais mpya zitafanyika Alhamisi saa sita mchana," mshauri mkuu wa Joseph Kabila anayehusika na masuala ya kidiplomasia, Barnaba Kikaya Bin Karubi, amesema kwa mujibu wa Kitengo cha Afrika cha Sauti ya Marekani (VAO Afrique).

Mshauri mwingine wa Rais Kabila pia amethibitisha taarifa hii, akisema sherehe itafanyika katika kwenye makao makuu ya Bunge la taifa, 'sherehe ambayo itahudhuriwa na marais kadhaa wa nchi za Afrika."

Ni kwa mara  kwanza nchi hiyo itashuhudia kuapishwa kwa rais mpya aliyechukua madaraka kwa njia ya amani kutoka kwa rais mwingine

"Ulimwengu utashuhudia siku hiyo sherehe kubwa ya kukabidhiana madaraka kwa amani, kinyume na jinsi wengi walivyofikira," amesema mshauri mwingine wa Kabila. Lakini hakuna taarifa rasmi iliyowekwa wazi kuhusu maelezo ya sherehe hiyo.

Timu ya rais mpya na ile ya rais anaye maliza muda wake wamekuwa wakijadili eneo na tarehe ya sherehe hiyo muhimu nchini DRC, vyanzo hivyo vimeongeza.

Mbali na marais hao wa nchi za Afrika, Ufaransa na Marekani zitawakilishwa katika sherehe hiyo na mabalozi wao. Siku ya Jumanne Rais mpya aliyechaguliwa Felix Tshisekedi alikutana na balozi wa Marekani.