Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Felix Tshisekedi aapishwa kama rais wa tano wa DRC, maandamano nchini Sudan yashika kasi, Maduro akabiliwa na hali ngumu kisiasa

Sauti 20:05
Rais mstaafu(kushoto) baada ya kuapishwa kwa rais mpya Felix Tshisekedi jijini Kinshasa, January 24 2019
Rais mstaafu(kushoto) baada ya kuapishwa kwa rais mpya Felix Tshisekedi jijini Kinshasa, January 24 2019 REUTERS/Olivia Acland

Mtazamo wako juma hili, imeangazia kuapishwa kwa Felix Tshisekedi kuwa rais wa tano ikiwa ni sherehe za kihistoria kwenye nchi hiyo ambayo imeshuhudia makabidhiano ya madaraka kati ya marais wawili wakiwa hai Januari 24 jijini Kinshasa, pia kwenye ukanda wa afrika mashariki tumegusia suala la kodi kama ambavyo wabunge wa EAC wakijadiliana wakati katika uga wa kimataifa mzozo wa kisiasa nchini Venezuela umezungumziwa kwa kirefu.