RWANDA-DRC-UHUSIANO-USALAMA

DRC / Rwanda: Makada wawili wa FDLR wasafirishwa Rwanda

Rais wa sasa wa Umoja wa Afrika Paul Kagame wakati wa mkutano kuhusu DRC, Alhamisi Januari 17, 2019.
Rais wa sasa wa Umoja wa Afrika Paul Kagame wakati wa mkutano kuhusu DRC, Alhamisi Januari 17, 2019. © EDUARDO SOTERAS / AFP

Viongozi wawili wa ngazi ya juu katika kundi la waasi wa Kihutu kutoka Rwanda FDLR waliokamatwa hivi karibuni wamesafirishwa nchini Rwanda. Miongoni mwa makada wa FDLR waliosafirishwa nchini Rwanda ni pamoja na msemaji wa kundi hilo, La Forge Fils Bazeye.

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka nchini DRC inamshtumu La Forge Fils Bazeye kupanga njama na makundi mengine ya waasi wa Rwanda, ikiwa ni pamoja na kundi la RNC, linaloongozwa na Kayumba Nyamwasa, kwa kufanya mashambulizi nchini Rwanda kutoka DRC.

`familia ya La forge Fils Bazeye wnasema kuwa wanahofia kuwa ndugu yao atauawa, huku wakisem akuwa kulikuepo na ahadi fulani kati ya DRC na Rwanda ambazo zilipelekea rais wa Rwanda ambaye pia rais wa Umoja wa Afrika kusitisha ziara ya ujumbe wa Umoja wa Afrika nchini DRC.

Bazeye alikamatawa kwenye eneo la mpakani huko Bunagana Desemba 15 mwaka jana akiwa pamoja na kada mwengine wa FDLR Theophile Abega.

Kabla ya Mahakama ya Katiba kuthibitisha matokeo ya uchaguzi Mkuu yaliyotangazwa na tume huru ya Uchaguzi, rais wa Rwanda, Paul Kagame, ambaye ni rais wa Umoja wa Afrika alitarajia kwenda mjini Kinshasa pamoja na ujumbe wa Umoja wa Afrika ambao ungeliwajumuisha viongozi wa nchi kadhaa. Wakati huo rais kagame aliomba mamlaka nchini DRC kusitisha kutangaza matokeo kamili ya uchaguzi wa urais. Hata hivyo Mahakama ya katiba ilifutilia mbali ombi hilo na kuamua kuthibitisha matokeo ya uchaguzi yaliyotangazawa na CENI.