DRC-YUMBI-USALAMA

Hali ya usalama yatisha katika mji wa Yumbi, DRC

Yumbi inapatikana katika jimbo la Mai-Ndombe, DRC.
Yumbi inapatikana katika jimbo la Mai-Ndombe, DRC. RFI

Hali bado ni tete katika mji wa Yumbi mkoa wa Mayi ndombe nchini DRC baada ya kutokea kwa machafuko baina ya watu kutoka makabila ya Banunu na Batende yaliogharimu maisha ya watu zaidi ya 900 kwa kipindi cha siku mbili zilizopita.

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa umesema makaburi ya pamoja zaidi ya 50 yamegundulika katika mkoa huo, ambapo taarifa zinasema yalichimbwa na mashirika ya kiraia kwa ajili ya kuwazika walipoteza maisha.

Kwa mujibu wa Patient Ligodi mwandishi wa habari wa RFI aliezuru katika eneo hilo, amesema hali bado ni tete asilimia kubwa ya watu wamekimbia makwao, huku majumba mengi yakiteketezwa moto.

Jeshi la Polisi waendesha doria na kutowa wito kwa watu walioimbia makwao kurejea wakati huu kukiw ana hofu ya kutokea kwa mashambulizi mengine mapya.

Yumbi ni miongoni mwa maeneo ambayo wananchi wake hawakushiriki uchaguzi wa desemba 30 kutokana na hali mbaya ya usalama.