BURKINA FASO-USALAMA

Kumi wauawa katika shambulio la kigaidi Burkina Faso

Kwenye ramani, kijiji cha Sikiré kaskazini mwa Burkina Faso.
Kwenye ramani, kijiji cha Sikiré kaskazini mwa Burkina Faso. Google Maps

Watu kumi wameuawa katika shambulio la kigaidi katika Kijiji cha Sikiré, kilomita ishirini kutoka Manispaa ya Arbinda, katika mkoa wa Soum, nchini Burkina Faso, kwa mujibu wa vyanzo vya polisi.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mashahidi washambuliaji waliwasili katika jiji hicho kwa pikipiki. Shambulio hilo ambalo lilitokea siku ya Jumapili asubuhi, siku ambayo watu walikuwa walifurukia sokoni.

Watu zaidi ya ishirini ambao walikuwa wamejihami kwa silaha waliwafyatulia risasi wakazi wa kijiji hicho. Kwa mujibu wa kiongozi aliyechaguliwa katika kijiji cha Sikire, washambuliaji hao "walikuwa wakizunguka kijiji hicho, huku wakiwafyatulia risasi wakaazi.

Washambuliaji hao pia waliipora na kuchoma moto maduka na biashara nyingine, kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho hakikutaja jina.

Januari 10, watu 12 waliuawa katika kijiji cha Gasseliki, kilomita 30 kusini mwa Arbinda, katika mkoa wa Soum, uliyowekwa chini ya hali ya dharura tangu mwanzoni mwa mwaka.