SENEGAL-SIASA-UCHAGUZI

Wanasiasa nchini Senegal watakiwa kunadi amani

Ousmane Sonko mmoja wa wagombea katika uchaguzu ujao Senegal.
Ousmane Sonko mmoja wa wagombea katika uchaguzu ujao Senegal. SEYLLOU / AFP

Mwezi mmoja kabla ya uchaguzi mkuu wa rais nchini Senegal, shirika linalo tetea haki za binadamu nchini humo Rado, limetoa wito wa utulivu katika kipindi hiki cha kampeni na kuwataka wapinzani kuendesha kampeni katika hali tulivu.

Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo limesema mpango wa upinzani katika kipindi hiki unazua hofu na hivyo inasisitiza kuwepo kwa kampeni za kistaarabu.

Hata hivyo Amadou Sall wa chama cha demokrasia nchini Sengal amesema shirika hilo linalotetea haki za binadamu limekosea mlengwa.

La rado na upinzani wanakubaliana kuwa kuondolewa kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi kwa Karim Wade na Khalifa Sall, hatuwa ambayo utawala unasema ni za kisheria na sio za kisiasa.