Jacob Zuma atajwa katika kashfa mpya ya rushwa
Imechapishwa:
Rais wa zamani wa Afrika Kusini amenukuliwa kwa mara ya kwanza Jumatatu wiki hii na tume ya uchunguzi inayohusika na kutoa mwanga kuhusu mashtaka ya rushwa alipokuwa madarakani.
Shahidi mmoja amemshtumu Jacob Zuma kwamba alikuwa akipokea rushwa kila mwezi kutoka kampuni ya usalama.
Kulingana na Angelo Agrizzi, afisa wa ngazi ya juu katika kampuni ya usalama ya Bosasa, rais wa zamani wa Afrika Kusini alikuwa akipokea euro 20,000 kila mwezi.
Angelo Agrizzi, ambaye katika siku nane za ushuhuda mbele ya tume ya uchunguzi tayari amewahusisha Wakurugenzi wakuu wa makampuni ya umma, waziri mmoja na waandishi wa habari.
Jacob Zuma alilipwa kwa fedha taslimu, ambazo ziliwekwa kwenye mkoba na kupelekwa na mtu maalumu, Dudu Myeni, ambaye wakati huo alikuwa kwenye nafasi ya kiongozi wa Wakfu wa Zuma Foundation na pia rais wa shirika la kitaifa la ndege.