CAMEROON-HAKI-SIASA

Kiongozi wa upinzani Cameroon Maurice Kamto akamatwa

Maurice Kamto, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha MRC nchini Cameroon, wakati wa mkutano wake wa kampeni Yaounde, Septemba 30, 2018.
Maurice Kamto, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha MRC nchini Cameroon, wakati wa mkutano wake wa kampeni Yaounde, Septemba 30, 2018. MARCO LONGARI / AFP

Kiongozi wa upinzani nchini Cameroon Maurice Kamto, ambaye alichukuwa nafasi ya pili katika uchaguzi wa urais wa mwezi Oktoba na ambaye anadai kuwa yeye ndio aliibuka mshindi, amekamatwa tangu Jumatatu jioni huko Douala.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa hii imethibitishwa na naibu kiongozi wa chama chake cha MRC, kwa mujibu wa shirika la Habari la AFP.

"Bw Kamto amekamatwa nyumbani kwa Albert Dzongang (mmoja wa wafuasi wake), alipelekwa polisi huko Douala," amesema Bw Simh, akithibitisha taarifa kutoka chanzo kilio karibu na mamlaka ya Douala.

Albert Dzongang na Christian Penda Ekoka, mwanauchumi, mfuasi wa Maurice Kamto, pia amekamatwa, Simh ameliambia shirika la Habari la AFP.

Hata hivyo mamlaka nchini Cameroon hawakuthibitish ataarifa hiyo.

Baada ya Kamto kukamatwa, watu 300 walikusanyika karibu na makaazi ya Bw Dzongang, kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa AFP. Vikosi vya usalama vilifyatua risasi hewani kwa kutawanya watu hao

Makada kadhaa wa chama cha MRC wamekamatwa tangu Jumamosi wiki iliyopita.

Chama hiocho kilitoa wito wa maandamano dhidi ya hatua ya Paul Biya ya kuwania muhula mwengine. rais Paul Biya, mwenye umri wa miaka 85 yuko madarakani kwa miaka 36. Tangu kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mwishoni mwa mwezi Oktoba, Maurice Kamto ameendelea kulalamika kuwa "ameibiwa kura".