LIBERIA-WEAH-UCHUMI

Rais Weah atetea rekodi yake baada ya kutimiza mwaka mmoja madarakani

Rais wa Liberia George Weah
Rais wa Liberia George Weah REUTERS/Thierry Gouegnon

Rais wa Liberia George Weah ametetea rekodi ya serikali yake, mwaka mmoja baada ya kuingia madarakani.

Matangazo ya kibiashara

Akiwahotubia raia wa nchi yake kwa zaidi ya saa mbili  siku ya Jumatatu usiku, rais Weah bingwa wa zamani wa mchezo wa soka , amesema rekodi ya serikali yake imeimarisha maisha ya raia wa nchi hiyo.

Weah, amepinga vikali upinzani kutoka kwa wapinzani wake ambao wanaona kuwa uchumi wa taifa hilo, umeendelea kushuka.

Viongozi wa upinzani na wale wa Makanisa, hata hivyo hawajaridhishwa namna rais huyo anavyoshughulikia suala la uchumi kwa madai ya kuweka mbele maslahi yake badala ya kuwatumikia raia wa nchi hiyo.

Hivi karibuni, Weah alishtumiwa kwa kuagiza kuchapishwa kwa noti mpya zenye thamani ya Dola Milioni 104 ambazo zilitoweka katika bandari na uwanja wa ndege wa Monrovia.