DRC-RAIS-KATUMBI-SIASA

Muungano wa kisiasa unaomuunga mkono Katumbi watambua rais Tshisekedi

Moïse Katumbi mwanasisa wa DRC
Moïse Katumbi mwanasisa wa DRC Yasuyoshi CHIBA / AFP

Jukwaa la kisiasa lijulikanalo kama Alter-nance pour la Republique AR ambalo linafahamika kuwa karibu na mwanasiasa Moise Katumbi ambae alikuwa amemuunga mkono Martin Fayulu katika uchaguzi wa rais, limetangaza kumtambua rais Felix Tshisekedi kama rais mpya nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa hiyo imetolewa na Jean Bertrand Ewanga ambae alikuw abega kwa bega na Martin fayulu wakati wa kampeni za uchaguzi.

Muungano wake Alternance pour le changement AR bado ni miongoni mwa vyama vinavyounda vuruguvu la pamoja kwa ajili ya mabadiliko linaloogozwa na Moise Katumbi Chapwe.

Wajumbe wengine kutoka upande wa Martin Fayulu kama vile Delly Sessanga aliamuwa kujiunga na upande wa Felix Tshisekedi wakati wa kampeni.

Hata hivyo mpasuko huo ndani ya muungano wa pamoja kwa ajili ya mabadiliko umeendelea kudhihirika huku Moise Katumbi akiw abado hajazungumzia lolote hadi sasa.

Upande wake Jean Pierre Bemba ambae alimuunga mkono Martin Fayulu kwa asilimia 100 amekanusha taarifa kwamba amejiunga na kambi ya Felix Tshisekedi.

Kupitia mtandano wake wa kijamii wa Twitter kwamba ni habari za uongo wakati huu katibu wake mkuu Eva Bazaiba akithibitisha kuwa chama chake cha MLC kitashiriki katika mkutano wa hadhara wa Feburuari  2 unaotarajiwa kufanywa na Martin Fayulu ambapo atatangaza mkkakati wake mpya.