DRC-SIASA-USALAMA

Fayulu awataka wafuasi wake kuendelea na vita vya kisiasa kwa amani

Mgombea wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo Martin Fayulu ametupilia mbali juhudi za rais mpya wa nchi hiyo Felix Tshisekedi ambaye ameonyesha nia ya kutaka maridhiano, akisema "unapopewa mkono ambao ni mchafu, hupaswi kupokea".

Martin Fayuluaendelea kupinga ushindi wa Felix Tshisekedi Tshilombo.
Martin Fayuluaendelea kupinga ushindi wa Felix Tshisekedi Tshilombo. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Mgombea wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo Martin Fayulu ametupilia mbali juhudi za rais mpya wa nchi hiyo Felix Tshisekedi ambaye ameonyesha nia ya kutaka maridhiano, akisema unapopewa mkono ambao ni mchafu, huupokei.

Akiwahutubia maelfu ya wafuasi wake kwa mara ya kwanza tangu kushindwa kwenye uchaguzi wa Desemba 30 mwaka jana, Fayulu amewaambia wafuasi wake waliokusanyika mjini Kinshasa mwishoni mwa juma lililopita, kuwa hatatumia fujo anapoendelea kupinga uchaguzi anaodai ulikumbwa na udanganyifu.

Martin Fayulu mbele ya wafuasi wake waliokusanyika mjini Kinshasa Februari 2, 2019.
Martin Fayulu mbele ya wafuasi wake waliokusanyika mjini Kinshasa Februari 2, 2019. JOHN WESSELS / AFP

Fayulu amesema jaji mmoja wa Mahakama ya Katiba amejitokeza na kuweka wazi kuhusu kilichofanyika,

Katika hatua nyingine Martin Fayulu ameongeza kuwa ameapa kushinikiza Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kutoheshimu amri kutoka kwa mtu anayedai hahuchaguliwa.