DRC-SIASA-USHIRIKIANO

Rais Tshisekedi alenga kuimarisha uhusiano kati ya DRC na mataifa jirani

Ikulu ya Rais mjini Kinshasa imethibitisha kuwa wiki hii rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi Tshilombo ataanza safari ya kwanza nje ya nchi ambapo atazuru mataifa kadhaa ikiwa ni pamoja na Angola, Kenya na Congo-Brazzaville.

Democratic Republic of Congo's Felix Tshisekedi swears into office during an inauguration ceremony as the new president of the Democratic Republic of Congo at the Palais de la Nation in Kinshasa, Democratic Republic of Congo January 24, 2019.
Democratic Republic of Congo's Felix Tshisekedi swears into office during an inauguration ceremony as the new president of the Democratic Republic of Congo at the Palais de la Nation in Kinshasa, Democratic Republic of Congo January 24, 2019. REUTERS/OLIVIA ACLAND
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hiyo ya Ikulu ya rais mjini Kinshasa imefahamisha kuwa rais Felix Tshisekedi anatarajiwa Kuianza safari yake ya kwanza baada ya kuchukua hatamu ya uongozi wa nchi nchini Angola ambapo Jumanne Ijayo atawasili mjini Luanda, kabla ya kuelekea Nairobi, nchini Kenya na Congo Brazzaville.

Lengo la ziara hiyo ni katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya DRC na mataifa jirani ziara inayofanyika kabla ya mkutano Mkuu wa Umoja wa Afrika katikati ya mwezi huu wa Februari, kulingana na chanzo hicho.

Ni zaira ya kwanza nje ya nchi hiyo tangu Tshisekedi, kuapishwa kuwa rais wa nchi hiyo Januari 24 ambapo Mahakama ya Katiba iliidhinisha ushindi wake Januari 20, baada ya Tume ya Uchaguzi (CENI) kumtangaza mshindi.

Baadhi ya nchi za Kiafrika na Ulaya zimekubali ushindi za rais huyo, ambaye sasa anakabiliwa na changamoto za kiusalama huku akiwa mbioni kuliunganisha taifa hilo la DRC.

Ifahamike katika sherehe za makabidhiano ya madaraka kati yake na rais aliyeondoka madarakani Joseph Kabila sherehe ambazo zilihudhuriwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pekee huku mataifa mengine yakiwatuma wawakilishi wao.