CAR-MAZUNGUMZO-USALAMA

CAR: Serikali na makundi 14 ya waasi watia sahihi mkataba wa amani Khartoum

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na shughuli za Amani, Kamishna wa Umoja wa Amani anaye husika na masuala ya Usalama na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan katika kikao cha ufunguzi wa mazungumzo huko Khartoum tarehe 24 Januari 2019.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na shughuli za Amani, Kamishna wa Umoja wa Amani anaye husika na masuala ya Usalama na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan katika kikao cha ufunguzi wa mazungumzo huko Khartoum tarehe 24 Januari 2019. ASHRAF SHAZLY / AFP

Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na makundi kumi na nne ya waasi wametia sahihi kwenye mkataba wa amani uliofikiwa baada ya siku kumi ya mazungumzo chini ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa.

Matangazo ya kibiashara

Hakuna anayejua kwa wakati huu yaliyomo kwenye mkataba huo.

Mengi huenda yakajulikana wakati wa kusainiwa kwa mkataba huo mjini Bangui katika siku chache zijazo.

Mkataba mpya wa amani kati ya serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na makundi 14 ya waasi umetiliwa saini katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum. Sherehe hiyo ilifanyika mbele ya rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadera na rais wa Sudan Omar al-Bashir, pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat.

Rais wa Chad alikuwa anatarajiwa, lakini hakuweza hakuweza kuwasili jijini Khartoum kwa sababu ya mkutano wa G5 Sahel uliopangwa kufanyika nchini Burkina Faso.

Makundi ya watu wenye silaha yanadhibiti karibu asilimia 80 ya nchi hiyo , makubaliano haya mapya - ambayo ni ya nane sasa- yameleta matumaini mapya kwa wananchi wa taifa hilo, hata kama kwa sasa hayajawekwa wazi.