Muungano wa upinzani wa Lamuka walaani wito wa chuki za kikabila dhidi ya Tshisekedi
Imechapishwa:
Muungano wa vyama vya upinzani Lamuka unaoongozwa na Martin Fayulu unalaani kile ulichokiita wito wa "chuki za kikabila" uliyotolewa na "watu wasiojulikana" kando ya mkutano wake siku ya Jumamosi mjini Kinshasa, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Katika mkutano huo ulioitikiwa na maelfu ya watu, kuna watu waliojitokeza na kuimba nyimbo za chuki dhidi ya jamii ya rais mpya, Felix Tshisekedi.
"Muluba zua ye Boma ye" (Muluba, mchukuwe na muue), waliimba watu hao kando na eneo kulikokuwa kukifanyika mkurano wa Lamuka, kulingana na video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
#Lamuka
Lamuka International (Officiel) (@_Lamuka) February 5, 2019
Le tribalisme n'a pas sa place en RDC. pic.twitter.com/cgA96XQx99
"Muungano wa vyama vya upinzani Lamuka haukufurahishwa na tabia ya baadhi ya watu wasiojulikana walitoa kauli za kuchochea chuki za kikabila kando ya mkutano wake wa tarehe 2 Februari," Mratibu wa muungano huo, Fidele Babala, ameandika katika taarifa.