COTE D'IVOIRE-SORO-SIASA

Spika wa bunge la Cote d'Ivoire aelekea kujiuzulu

Guillaume Soro, hapa ilikuwa Julai 20, 2017 katika uwanja wa ndege wa Abidjan.
Guillaume Soro, hapa ilikuwa Julai 20, 2017 katika uwanja wa ndege wa Abidjan. © Sia KAMBOU / AFP

Kikao kisichokuwa cha kawaida cha bunge la Cote d'Ivoire kimeitishwa leo Ijumaa, Februari 8 katika hali ya kujadili hatima ya Spika wa bunge Guilluame Soro, ambapo inaelekea kuwa huenda akachukuwa hatua ya kujiuzulu leo Ijumaa.

Matangazo ya kibiashara

Hatua ya kujiuzulu kwa Guillaume Soro ilitangazwa mwishoni mwa mwezi Januari na rais Alassane Ouattara. Wawili hao walikubaliana kuhusu suala hilo, baada ya Guillaume Soro kukataa kujiunga na chama kipya cha RHDP.

Suala hili la kujiuzulu kwa Guillaume Soro limekuwa gumzo mjini Abidjan. Spika wa Bunge na rais Alassane Ouattara walikutana angalau mara mbili tangu mwanzoni wa mwaka huu ili kujadili suala hilo la kujiuzulu kwenye nafasi ya spika wa bunge.

Alassane Ouattara mwenyewe alitamka mbele ya waandishi wa habari tarehe 28 Januari mwaka huu akisema kuwa: "Guillaume Soro atajiuzulu mnamo mwezi Februari, tumekubaliana, suala hilo limekwisha patiwa ufumbuzi.