UN-AU-GUTERESS

Guteress awaambia viongozi wa nchi za Magharibi waige Afrika kuhusu wakimbizi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres SIMON MAINA / AFP

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mataifa ya Magharibi yana mengi ya kujifunza kutoka barani Afrika kuhusu namna ya kuwashughulikia wakimbizi.

Matangazo ya kibiashara

Guteress amewaambia viongozi wa Afrika wakati wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kuwa wanafanya vema kwa kuacha wazi mipaka ya mataifa yao kwa wakimbizi kutafuta hifadhi kwa sababu ya sababu mbalimbali.

Mkuu huyo wa UN ameongeza kuwa, bara la Afrika limeendelea kuwakarimu wakimbizi licha ya bajeti ndogo ya kifedha waliyonayo kinyume na mataifa ya Magharibi ambayo limekuwa likiwazuia wahamiaji na wakimbizi kuingia katika nchi zao.

Bara la Afrika, limewapa hifadhi zaidi ya robo ya wakimbizi wote duniani, na wale waliokimbia kutoka makwao, wanaokaridiwa kufikia Milioni 20.

Kauli hii imekuja wakati huu bara la Afrika likiendelea kushuhudia idadi kubwa ya waafrika wakiendelea kuhamia barani Ulaya na kwa bahati mbaya wengi wao kuzama katika Bahari ya Atlantic, Pwani ya Libya.