DRC-RWANDA-SIASA

Rais Tshisekedi na Kagame wakutana jijini Addis Ababa

Rais mpya wa Jamhuri  ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi Tshilombo amekutana  na rais wa Rwanda Paul Kagame ambaye alikuwa ametilia shaka kuchaguliwa kwake  katika uchaguzi mkuu wa urais wa Desemba 30 mwaka 2018.

Rais wa DRC Felix Tshisekedi (Kushoto) akishauriana na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame (Kulia) baada ya kukutana pembezoni mwa mkutano mkuu w a AU jijini Addis Ababa nchini Ethiopia
Rais wa DRC Felix Tshisekedi (Kushoto) akishauriana na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame (Kulia) baada ya kukutana pembezoni mwa mkutano mkuu w a AU jijini Addis Ababa nchini Ethiopia @UrugwiroVillage Following Following @UrugwiroVillage More
Matangazo ya kibiashara

Pembezoni mwa mkutano mkuu wa viongozi wa Afrika jijini Addis  Ababa,viongozi hao wawili wa nchi jirani, walijadiliana kwa zaidi ya saa mbili  kuhusu masuala mbalimbali hususan kuhusu ujirani mwema, ushirikiano kati ya nchi zao mbili.

Januari 17 Paul Kagame akiwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika aliiomba mahakama ya kikatiba nchini DRC kutotangaza matokeo ya uchaguzi kabla ya kutuma ujumbe wa umoja huo  kwa ajili ya mashauriano, lakini Mahakama iliendelea na kumtangaza Tshisekedi mshindi.

Rwanda nchi ndogo yenye ukumbwa wa Kilomita ya mraba elfu 26 na DRC nchi kubwa yenye ukubwa wa Kilomita Milioni 2.3.

Nchi ya  Rwanda inaingia ndani ya DRC  mara 90. Nchi hizi kwenye uhusiano mbaya tangu kutokea kwa mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994.

Kinshasa imekuwa ikiituhumu Rwanda kupora rasilimali zake hususan madini ya Coltan kaskazini mwa nchi yake  wakati Kigali ikisema inawalenga kundi la wahutu wa FDLR waliokimbilia mashariki wa nchi hiyo.

Jijini Addis Abeba rais Tshisekedi amekutana pia na mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini ambapo wamejadili kuhusu kurejeshwa jijini Kinshasa kwa mwakilishi wa Umoja huo aliyefukuzwa mwezi Desemba mwaka 2018.