LIBYA-AU-UN

Umoja wa Afrika waitisha mkutano wa Kimataifa kuijadili Libya

Ofisi ya Wizara ya Mambo ya nje jijini Tripoli nchini Libya
Ofisi ya Wizara ya Mambo ya nje jijini Tripoli nchini Libya REUTERS/Hani Amara

Umoja wa Mataifa umeitisa mkutano wa Kimataifa kuangazia hali ya kisiasa na usalama nchini Libya mwezi Julai.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo pia unalenga kushinikiza nchi hiyo kuandaa Uchaguzi Mkuu nchini Libya mwezi Oktoba mwaka huu.

Taarifa ya Umoja huo imesema kuwa, mbali na Umoja wa Afrika, wadau wengine kutoka Umoja wa Mataifa wanatarajiwa kushiriki.

Tangazo hili limetolewa baada ya Abdel Fattah al-Sisi rais wa Misri kuchukua unyekiti wa Umoja huo na kusisitiza kuwa, matatizo ya Afrika lazima, yashughulikiwe na waafrika wenyewe.

Libya imekuwa katika mgogoro wa kiuchumi na kisiasa tangu mwaka 2011, baada ya kuuawa kwa kiongozi wa nchi hiyo Muamar Kadhafi.

Serikali ya Libya inayoongozwa na rais Fayez al-Sarraj inatambuliwa Kimataifa lakini inapata upinzani kutoka kwa Khalifa Haftar anayeongoza waasi.