AFRIKA KUSINI-COSATU-UCHUMI

Afrika Kusini: Cosatu waitisha mgomo dhidi ya serikali

Majengo ya chama kikuu cha wafanyakazi Afrika Kusini, Cosatu, Johannesburg.
Majengo ya chama kikuu cha wafanyakazi Afrika Kusini, Cosatu, Johannesburg. © MUJAHID SAFODIEN / AFP

Chama tawala nchini Afrika Kusini, ANC, kinagubikwa na hali ya sintofahamu kwa sasa. Chama kikuu cha wafanyakazi nchini humo Cosatu, kimeitisha mgomo wa kitaifa dhidi ya serikali Jumatano wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Cosatu inaomba kufutwa kwa muswada wa rais Cyril Ramaphosa, ambao unataka kurekebisha na kubinafsisha baadhi ya makampuni ya umma.

Cosatu ni mmoja ya washirika wa kihistoria wa chama tawala ANC, na inashiriki katika muungano serikalini. wito huo wa Cosatu ni ishara kubwa kwa ANC ikiwa imesalia miezi mitatu kabla ya uchaguzi wa urais.

Kilichosababisha maelfu ya wafanyakazi wa Afrika Kusini wanaingia mitaani ni mpango wa urekebishaji wa kampuni ya umeme ya Eskom. "Tunaona mpango huu kama njia ya kuwezesha ubinafsishaji wa Eskom na hatua za kibaguzi. Na wale ambao watakabiliwa na hali mbaya ya maisha ni wafanyakazi wa kawaida, " amesema Thabang Sonyathi, mweka hazina wa Cosatu mjini Johannesburg.

Kwa mujibu wa Thabang Sonyathi, tabia ya ANC imewachosha wanachama wa Cosatu, ambao wanaweza kubadilisha kura zao mwezi Mei: "Watu wenye hasira wameendelea kuongezeka miongoni mwa wanachama wetu na wafanyakazi kwa ujumla.

Cosatu haijaachia ngazi, na imeandaa mgomo mwengine wa kitaifa wiki ijayo.