COTE D'IVOIRE-GBAGBO-ICC-HAKI

Kauli ya Ouattara kuhusu Ocampo yazua mjadala Cote d'Ivoire

Mnamo Oktoba 15, 2011, Alassane Ouattara alimpokea Luis Moreno-Ocampo katika makazi yake binafsi huko Riviéra Golf.
Mnamo Oktoba 15, 2011, Alassane Ouattara alimpokea Luis Moreno-Ocampo katika makazi yake binafsi huko Riviéra Golf. © www.gouv.ci

Kauli ya rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara kuhusu kukutana na mwendesha mashitaka wa zamani wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) imezua mjadala mkubwa nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Jumatatu wiki hii, rais Ouattara akihojiwa na RFI alisema kuwa alizungumza tu "mara moja au mara mbili" na mwendesha mashitaka wa zamani wa ICC Luis Moreno Ocampo.

Kwa mujibu wa vyanzo rasmi, wawili hawa walikutana mara kadhaa, hasa kuhusu faili ya Laurent Gbagbo, na mazungumzo kati ya mamlaka ya Cote d'Ivoire na ICC yalifanyika mara kadhaa.

Jumatatu asubuhi Februari 11, katika mahojiano na RFI, rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara, alihakikisha kwamba, hamtambui "hata kidogo" mwendesha mashitaka wa zamani wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, Luis Moreno Ocampo.

Alibaini kwamba alizungumza naye "kwenye simu mara moja au mara mbili".

Hata hivyo Alassane Ouattara na Luis Moreno Ocampo walikutana mara kadhaa. Kwa mfano, Novemba 26, 2011, siku nne kabla ya Laurent Gbagbo kuhamishwa kwenda Hague.

Kulingana na utafiti wa Mediapart na European Investigative Collaboration uliochapishwa mwezi Oktoba 2017, ofisi ya rais wa Cote d'Ivoire iliwasiliana na mmoja wa viongozi wa kitengo cha ofisi ya mwendesha mashitaka, na kupendekeza kukutana mjini Brussels mnamo Novemba 22, ("Apero offert by the President to the Prosecutor," maneneo yaliyoandikwa kwenye hati ya ndani ya Mahakama), au Novemba 26 mjini Paris, ambapo Alassane Ouattara ana makazi yake.

Kwa mujibu wa ripoti ya mfanyakazi wa Mahakama, Rais wa Cote d'Ivoire alitaka kujua matokeo ya kesi ya Laurent Gbagbo, na "kujua ujumbe gani anaweza kutoa kwa wanadiplomasia ambao alitarajia kukutana nao huko Brussels".

Mwendesha mashitaka Ocampo na rais Ouattara hatimaye walikutana mjini Paris Novemba 26, saa 11:30. Siku hiyo, shirika la habari la Express, lilibaini kwamba wawili hao wanatarajia kutajadili kuhusu kuhamishwa kwa Laurent Gbagbo kwenda Hague. Wakati wa mchana, Ocampo pia alikutana na afisa mwandamizi wa wizara ya mamabo ya nje ya Ufaransa Quai d'Orsay katika kanda ya Afrika, Stéphane Gompertz, katika hoteli yake, mtaa wa Montalembert mjini Paris. Siku nne baadaye, tarehe 30 Novemba, Gbagbo alifikishwa mbele ya mahakama ya Korhogo, kaskazini mwa Cote d'Ivoire, ambapo alikuwa akizuiliwa tangu kukamatwa kwake mwezi Aprili 2011. Wakati huo alifahamishwa kuwa anatafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC). Kisha, Rais wa zamani wa Cote d'Ivoire alisafirishwa mapem aasubuhi kutoka mji wa Kouakou Fofie hadi uwanja wa ndege, kabla ya kusafirishwa na ndege ya rais hadi Uholanzi.

Hata hivyo Rais Ouattar amefutilia mbali madai hayo.