NIGERIA-UCHAGUZI-SIASA

Wananchi wa Nigeria kumchagua rais wao mpya Februari 16

Wananchi wa Nigeria wanatarajia kumchagua rais wao mpya.
Wananchi wa Nigeria wanatarajia kumchagua rais wao mpya. guardian.ng

Nigeria, taifa kubwa, lenye wakaazi wengi barani Afrika linajiandaa kumpata rais mpya na bunge jipya, Februari 16. Nigeria ina wakazi milioni 180.

Matangazo ya kibiashara

Nigeria ambayo inaongoza kwa uchumi Kusini mwa Jangwa la Sahara, ni nchi muhimu kwa bara la Afrika.

Nigeria ambayo inazungukwa na Benin, Cameroon, Niger na Chad, ni nchi yenye nguvu katika kanda ya Afrika Magharibi.

Nigeria ina jukumu muhimu katika Umoja wa Afrika (AU) na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika (ECOWAS), ambayo makao yake makuu yanapatikana Abuja.

Pia ni mchangiaji mkubwa, kwa askari, katika shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa.

Nigeria ambayo inakabiliwa na mashambulizi ya Boko Haram, imeimarisha ushirikiano wake na nchi nyingine za kanda, kwa nyanja ya usalama.

Kwa sababu zote hizi, Afrika inasubiri kuona kitakachotokea kwenye uchaguzi wa Februari 16.

Wanigeria wanatarajia kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu. Watapiga kura kumchagua kati ya Muhammadu Buhari au mgombea mwingine.

Muhammadu Buhari, rais wa sasa, anawania muhula wa pili. Mwaka 2015, alichaguliwa baada ya kuahidi kutokomeza kundi la Boko Haram, kupambana dhidi ya rushwa na kuimarisha uchumi. Mshindani mkubwa wa Buhari ni Atiku Abubakar, mwenye umri wa miaka 72.