NIGERIA-UCHAGUZI-BUHARI-ABUBAKAR

Wagombea Urais nchini Nigeria wajigamba kuwa Tayari kwa Uchaguzi

Major candidates in 2019  Nigeria presidential election, Muhammadu Buhari and Atiku Abubakar
Major candidates in 2019 Nigeria presidential election, Muhammadu Buhari and Atiku Abubakar RFI Hausa

Kampeni za Uchaguzi Mkuu nchini Nigeria zilimalizika ambapo wapiga kura Milioni 84 wanatarajiwa kupiga kura Jumamosi Februari 16 kumchagua rais wao mpya kati ya Muhammadu Buhari na wagombea wengine 71.

Matangazo ya kibiashara

katika kambi inayomuunga mkono kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Atiku Abubakar Mjini Lagos wafuasi wake wamejitokeza kumuunga mkono.

Walifanya kampeni za mwisho wakiwa na imani kuwa, mgombea wao atashinda.

“Tunamhitaji Atiku aje atuongoze sasa hivi, tumechoka kuteseka, tunawaomba sana Wanigeria wampigie kura Atiku, uchumi wetu utaimarika na mambo yatakuwa mazuri, ” amesema mmoja wa mfuasi wa abubakar akihojiwa na mwandishi wetu Victor Abuso akiwa nchini Nigeria.

Kwa upande wa chama tawala cha APC, wao walitumia matarumbeta katika eneo la Ikoyi, katikati mwa mji huu, kumwombea rais Buhari kura.

Mmoja wa wafuasi hao anaamini kuwa rais Buhari anastahili kurejea tena madarakani.

“Buhari anajenga msingi, msingi wa maendeleo, ukweli na kupinga ufisadi, sababu hizi ndizo zilizotufanya kuacha kazi zetu na kuja hapa kumuunga mkono ili Nigeria iendelee” Amesema mmoj awa wafuasi wa Buhari.

Kuelekea uchaguzi wa kesho, rais Buhari ambaye anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa mpinzani wake Atiku Abukakar.

Atiku naye alituma ujumbe wake wa mwisho kabla ya siku ya upigaji kura.

Wagombea zaidi 70 wanawania urais, lakini ushindani ni kati ya rais Muhammadu Buhari na makamu wa rais wa zamani Atiku Abubakar.