NIGER-USALAMA

Afisa mwandamizi wa jeshi la Niger na dereva wake wauawa Dirkou

skari wa Nigeria wakipiga doria katika eneo la Ayorou, kaskazini-magharibi mwa Niamey, Niger (picha ya kumbukumbu).
skari wa Nigeria wakipiga doria katika eneo la Ayorou, kaskazini-magharibi mwa Niamey, Niger (picha ya kumbukumbu). © ISSOUF SANOGO / AFP

Mkuu wa kambi kubwa ya jeshi katika Jangwa la Tenere huko Dirkou ameuawa katikia shambulio la kuvizia. Taarifa hii imethibitishwa na makao makuu ya jeshi la Niger. Aliuawa katika shambulio la kuvizia huko Oufagadoute.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lilitekelezwa na kundi la watu waliojihami kwa silaha za kivita. Dereva wake pia ameuawa. Kamanda Lamine Mohamedine ni afisa mwandamizi katika jeshi na alisomea masuala ya jeshi katika Chuo Kikuu cha Algiers, nchini Algeria.

Jeshi limesema kuwa linawatafuta waliohusika na mauaji hayo.

Kamanda Lamine Mohamedine alikuwa anarudi akitokea katika mkutano uliofanyika jijini Niamey Jumatatu wiki hii wakati msafara wake ulishambuliwa kati ya Agadez na Dirkou kaskazini mwa nchi. Alikuwa katika gari dogo la mbele wakati watu hao wenye silaha waliposhambulia. Kamanda na dereva wake wote wameuawa.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa awali, washambuliaji walikuwa wamevalia sare za jeshi na walikuwa katika magari 14 yenye rangi ya jeshi la Chad, huku wakibebelea silaha za kivita.

Vyanzo vya kiusalama vinabaini kwamba washambuliaji huenda ni watoro wa jeshi la Chad, labda askari wa zagawa. Uwezekano mwengine, washambuliaji hao wanaweza kuwa waasi wa Chad walionusurika katika mashambulizi ya anga ya jeshi la Ufaransa wiki mbili zilizopita, kaskazini mashariki mwa Chad.

Hata hivyo kwa kifo cha kamanda Lamine Mohamedine, jeshi la Niger limepoteza moja ya nguvu muhimu kwa jeshi lake katika eneo ambalo hali ni tete kati ya wimbi la wahamiaji, walanguzi wa madawa ya kulevya na magaidi.