BURUNDI-SOMALIA-USHIRIKIANO

Rais wa Somalia Mohamed Farmajo azuru Burundi

Wanajeshi wa Burundi waliojiunga na kikosi cha Amisom, wakipiga doria katika wilaya ya Deynille, nchini Somalia, Novemba 18 mwaka 2011.
Wanajeshi wa Burundi waliojiunga na kikosi cha Amisom, wakipiga doria katika wilaya ya Deynille, nchini Somalia, Novemba 18 mwaka 2011. Reuters

Rais wa Somalia Mohamed Farmajo ambaye amekamilisha ziara yake ya siku mbili nchini Burundi amekutana na rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza.

Matangazo ya kibiashara

Ziara hiyo inakuja wakati ujumbe wa Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) unajiandaa kuondoa maelfu ya askari wa Burundi katika kikosi chake mwishoni mwa mwezi huu.

Baada ya mkutano wao, rais wa Burundi Pierre Nkurunziza na mwenzake wa Somalia Mohamed Farmajo wametoa wito wa mkutano wa haraka wa viongozi wa nchi zinazochangia askari wa AMISOM, nchini Somalia.

Ombi hilo linahusiana na tangazo la kuondoa maelfu ya askari wa Burundi nchini Somalia ifikapo Februari 28 mwaa huu, hatua ambayo serikali ya Burundi inailalamikia.

Kwa upande wa serikali ya Burundi, kupelekwa kwa askari wake nchini Somalia ni katika hali ya kupata fedha.

Serikali ya Burundi imekuwa ikishtumiwa kukwepesha sehemu ya mishahara, inayolipwa kwa dola na ambayo kwa kiasi kikubwa inatolewa na Umoja wa Ulaya.

"Kutokana na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na hali ya kisiasa nchini, ni aibu, chanzo cha kidiplomasia kimesema. Kuondoa askari elfu moja ni njia ya kuadhibu viongozi wa nchi hiyo".

Marais wa Somalia na Burundi pia wameomba AMISOM kuendelea kusimamia mamlaka yake kamili. Pia wameahidi kuendesha operesheni dhidi ya kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Al Shabab haraka iwezekanavyo, kwa kusubiri majeshi ya Somalia yajiimarishe.

Hatimaye, Mogadishu inapaswa kuchukuwa nafasi ya AMISOM, lakini mpango wa kuondoa askari wa Afrika unachelewa. "Mpango huo umetelekezwa kabisa," mwanadiplomasia mmoja amesema. Sote tulikuwa na shauku kwa mara ya kwanza lakini mambo yamekwama".