NIGERIA-UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi Nigeria: Tume ya Uchaguzi yawatoa hofu wapiga kura

Mahmood Yakubu, mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Nigeria, Februari 20, 2019 Abuja.
Mahmood Yakubu, mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Nigeria, Februari 20, 2019 Abuja. © REUTERS/Afolabi Sotunde

Nigeria inaendelea kukumbwa na mgogoro wa uchaguzi baada ya Uchaguzi Mkuu uliotarajiwa kufanyika Jumamosi Februari 16 kuahirishwa kwa wiki moja.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na tangazo la Tume ya Uchaguzi (INEC) Uchaguzi Mkuu utafayika Jumamosi Februari 23, 2019.

Hata hivyo ikiwa zimesalia siku tatu kabla ya kufanyika uchaguzi huo, tume ya uchaguzi inakabiliwa na shinikizo. Vyama viwili vikuu ambavyo mwezi mmoja uliopita viliwataka wafuasi wao kuwa watulivu, sasa vinaendesha vita vya maneno makali. Vyama hivyo vinaishtumu Tume ya Uchaguzi (INEC) kushindwa kuandaa uchaguzi huru, wa kuaminika na wa wazi.

Wakati huo huo INEC imeahakikisha kuwa uchaguzi utafanyika Jumamosi Februari 23.

Tume ya Uchaguzi inashtumiwa kuegemea upande wa upinzani, huku upinzani ukiishtumu kuwa chini ya udhibiti wa serikali, Chama tawala cha All Progressives Party, APC, na chama cha upinzani cha People's Democratic Party, PDD, vinashangazwa ana uamuzi wa INEC wa kusogeza mbele Uchaguzi Mkuu dakika chache kabla ya zoezi la kupiga kura kuanza Jumamosi ya wiki iliyopita.

Tume ya uchaguzi imesema imefikia uamuzi wake baada ya kutafakari kwa kina kuhusu masuala ya usafirishaji wa vifaa na kufika kwa wakati kwenye vituo, changamoto ambayo tume hiyo inasema isingewezekana kuwa na uchaguzi huru, haki na wakuaminika.

Hata hivyo mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, INEC, Mahmood Yakubu, akizungumza na wanahabari usiku wa kuamkia siku ya upigaji kura, alisema kwa ratiba ilivyo, isingewezekana tena kwa uchaguzi huo kufanyika kwa wakati.