CONGO-USALAMA-HAKI

Amnesty yaomba uchunguzi kuhusu kifo cha Servais Magloire Babissat

Pointe noire, mji mkuu wa kiuchumi wa Congo Brazzaville.
Pointe noire, mji mkuu wa kiuchumi wa Congo Brazzaville. RFI/G.NGOSSO

Shirika la kimataifa la haki za binadamu Amnisty International limeitaka serikali ya Congo Brazzaville kuweka wazi mazingira ya kifo cha aliyekuwa kamanda mkuu wa kikosi cha wanajeshi wa nchi kavu, cha jeshi la nchi hiyo huko Pointe Noire, servais Magloire Babissat.

Matangazo ya kibiashara

Amnesty imesema January 2019 mwili wa Babissat ulikutwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti, wakati familia yake ilijuwa kwamba anashikiliwa gerezani na vikosi vya usalama, tangu kukamatwa kwake mwezi Februari mwaka wa 2016.

Ripoti ya Amnesty imeenda mbali na kusema kuwa miaka mitatu tangu kukamatwa kwake Jenerali Servais Magloire Babissa hakupewa ruhusa ya kukutana na familia yake, wala hapakuwa kesi yoyote mbele ya mahakama dhidi yake.

Servais Magloire Babissat alifariki dunia kaiwa gereza usiku wa tarehe 19 kuamkia 20 Januri mwaka huu.

Alikuwa akiishi Siafoumou na alikuwa mkuu wa kanda ya kwanza ya ulinzi ya Pointe-Noire, alipokamatwa na kufungwa Februari 5, 2016.

Mwili wake ulipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti, lakini mjomba wake, ambaye ni kiongozi wa familia na watoto wake hawakuruhusiwa kuona mwili.

Amnesty imeomba mamlaka nchini Congo-Brazzaville kuanzisha haraka uchunguzi huru na usio na upendeleo kuhusu mazingira ya kifo cha afisa huyo wa ngazi ya juu katika jeshi.