SENEGAL-SIASA-UCHAGUZI

Senegal yasubiri matokeo ya uchaguzi

Zoezi la kuhesabu kura katika kituo cha kupigia kura jijini Dakar, Februari 24, 2019.
Zoezi la kuhesabu kura katika kituo cha kupigia kura jijini Dakar, Februari 24, 2019. © REUTERS/Zohra Bensemra

Siku moja baada ya uchaguzi wa urais nchini Senegal, wapiga kura wanasubiri na wametoa wito kwa wanasiasa kuepukana na kauli mbovu zinazoweza kuchochea machafuko. Licha ya misimamo tofauti, matokeo rasmi ya uchaguzi bado hayajatangazwa.

Matangazo ya kibiashara

Zoezi la kuhesabu kura limeanza katika maeneo mbalimbali nchini Senegal. Zoezi hili lilianza baada ya kura kutoka vituo mbalimbali kukusanywa Jumapili jioni.

Jumapili jioni Waziri Mkuu wa Senegal mbele ya waandishi wa habari kwamba rais anaye maliza muda wake Macky Sall ameshinda uchaguzi. Kauli ambayo ilizua mvutano, wakati upinzani ukidai kwamba kulingana na matokeo yaliyokusanywa, wanajiandaa kumuuangusah macky Sall katika duru ya pili ya uchaguzi.

Matokeo ya awali yanatarajiwa kutangazwa Jumanne wiki hii. na matokeo kamili yatatangazwa na Mahakama ya Katiba siku ya Ijumaa usiku wa manane.