DRC-KAMAKO-USALAMA-MAUAJI

Wanamgambo 19 wa Kamuina Nsapu wauawa Kasaï

Tangu Felix Tshisekedi kuchukuwa hatamu ya uongozi wa nchi, wanamgambo wengi wa Kamuina Nsapu wameweka chini silaha zao.
Tangu Felix Tshisekedi kuchukuwa hatamu ya uongozi wa nchi, wanamgambo wengi wa Kamuina Nsapu wameweka chini silaha zao. © Sonia Rolley/RFI

Wanamgambo Kumi na Tisa wa Kamuina Nsapu wameuawa na jeshi la DRC, baada ya makabiliano makali kati ya wanamgambo hao na jamii ya Tetela. Tukio hilo lilitokea siku ya Jumapili Februari 24.

Matangazo ya kibiashara

Wanamgambo wa Kamuina Nsapu, jina la kiongozi wa kijadi ambaye aliasi dhidi ya utawala wa Kishasa, wamekuwa wamekusanywa katika na kijiji cha Kamako huko Kasai baada ya kuweka chini silaha zao. Lakini makabiliano yalizuka Jumapili, Februari 24 kati ya wanamgambo hao, kutoka jamii ya Waluba, na jamii ya Tetela.

Baada ya Felix Tshisekedi kutoka mkoa wa Grand Kasai, kuchukuwa hatamu ya uongozi wa nchi wanamgambo wengi wa Kamuina Nsapu waliamua kuweka chini silaha wiki iliyopita katika kijiji cha Kamako.

Wanamgambo hao na familia zao walikusanyika huko Kamako. Kwa mujibu wa mashahidi, wanamgambo hao na familia zao walikuwa hawapati msaada wowote kutoka serikali au mashirika ya kihisani.

Kutokana na hali hiyo, siku ya Jumapili waliamuawa kwenda sokoni, lakini kwa mujibu wa wenyeji wa Kamako, hali hiyo haikutazamwa kwa jicho la heri na watu kutoka jumuiya ya Tetela.

Kwa mujibu wa amwanaharakani wa haki za binadamu katika kijiji cha Kamako, mkuu wa jamii ya Tetela alipinga vikali wanamgambo wa Kamuina Nsapu kupewa huduma yoyote kwenye soko hilo. Kulingana na chanzo hiki, wanamgambo hao wa zamani waliamua kumkamata na kumpeleka kwenye makao makuu yao.

Jeshi liliingilia kati. Watu takribani 19 waliuawa, ikiwa ni pamoja na mwanamke mmoja na watoto saba, kwa mujibu wa vyanzo kutoka Kamako. Pengine zaidi, kwa sababu kwa mujibu wa vyanzo kadhaa, baada ya jeshi kuingilia kati, watu kutoka jamii ya Tetela waliingia mitaani huku wakijihami kwa visu na mapanga,na kushambulia watu wanaongea lugha ya Kiluba, kwa mujibu wa mashahidi.

Baada siku nzima ya machafu (mchana na usiku), Jumatatu jioni, watu 500 kutoka jamii hiyo ya Tetela walitoroka makaazi yao na kukimbilia karibu na kambi ya askari wa Umoja w mataifa nchini DRC (MONUSCO) huko Kamako. Kwa sasa hali imerejea kuwa tulivu lakini bado kuna wasiwasi.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa (MONUSCO) na gavana wa mkoa wa Grand Kasai wanatarajiwa kwenda kamako Jumanne hii, Februari 26.