NIGERIA-UCHAGUZI-SIASA

Muhammadu Buhari aibuka mshindi wa uchaguzi wa urais Nigeria

Rais anayemaliza muda wake (hapa siku ya kupiga kura Februari 23) achaguliwa tena kwa muhula mwingine wa miaka minne.
Rais anayemaliza muda wake (hapa siku ya kupiga kura Februari 23) achaguliwa tena kwa muhula mwingine wa miaka minne. © REUTERS/Afolabi Sotunde/File Photo

Rais anayemaliza muda wake nchini Nigeria Muhammadu Buhari ameshinda kiti cha urais katika uchaguzi wa urais uliofanyika Jumamosi Februari 23. Kulingana na matokeo ya awali yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi (INEC), Buhari amepata 56% ya kura.

Matangazo ya kibiashara

Muhammadu Buhari amechaguliwa tena kuingoza nchi hiyo kwa mihula minne ijayo.

Hata hivyo awali upinzani ulilalama kwamba kuna njama ya kuiba kura na kubaini kwamba hautokubali matokeo ya uchaguzi

Muhammadu Buhari ameshinda kwa kishindo katika majimbo ya Kaskazini, ambapo wakazi wao majimbo hao ni wengi. katika Jimbo la Kano, amepata kura milioni 1.4, sawa na katika Jimbo la Katsina ambako anazaliwa.

Pia amepata ushindi mkubwa katika Majimbo ya Bauchi, Borno, Yobe, Zamfara na Kaduna.

Buhari mwenye umri wa miaka 76 amemshida mpinzani wake mkuu na aliyekua makamu wa rais bwana Atiku Aboubakar.

Chama cha Buhari kimeshinda majimbo 19 kati ya 36 , wakati chama cha upinzani cha PDP wakishinda majimbo 17.

Asilimia 35 tuu ya wapiga kura walijitokeza , baadhi wafuasi wa Buhari tayari wameingia mtaani kushangilia.

Buhari alichaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2015 akiwa ni kiongozi wa kwanza wa upinzani kukalia kiti cha urais.