DRC-M23-USALAMA

Waasi zaidi ya 60 wa zamani wa M23 warejea nyumbani DRC

wapiganaji wa kundi la zamani la M23, Februari 2014.
wapiganaji wa kundi la zamani la M23, Februari 2014. AFP PHOTO/ ISAAC KASAMANI

Serikali ya Uganda juma hili imeanza kuwarejesha nchini DRC wapiganaji wa zamani wa kundi la M23 pamoja na familia zao, ikiwa ni sehemu ya makubaliano kati ya waasi hao wa zamani na Serikali ya Uganda na DRC kurejea nyumbani kwa hiari.

Matangazo ya kibiashara

Jumanne ya wiki hii Uganda iliwarejesha wapiganaji zaidi ya 70, utawala wa Kampala ukisema wengi wa wapiganaji hao wamekubali kwa hiari kurejea pamoja na familia zaidi.

Wapiganaji hawa wanarejea nyumbani ikiwa ni miaka 5 tangu kundi hilo lishindwe vita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Wapiganaji hao walioandamana na jamaa zao kumi wamesafirishwa kwa ndege ya Umoja Mataifa kutoka uwanja wa Entebbe Jumanne Februari 26 kuelekea nchi yao.

Hatua ya kuwarejesha nyumbani imechukuliwa chini ya mpango wa utekelezaji wa makubaliano yaliofanyika mwaka 2013 ukiwa moja kati ya mikakati ya kutatua mzozo wa vita katika eneo la maziwa makuu.

Watu hao wataamua kurejeshwa katika maisha ya kiraia au kuingizwa katika vuyombo vya usalama na ulinzi, kwa mujibu wa chanzo cha serikali ambacho hakikutaja jina lake.