Pata taarifa kuu
CAR-SIASA-USALAMA

Mkataba wa amani waingiliwa na mvutano Jamhuri ya Afrika ya Kati

Mmoja wa washiriki wa makundi ya waasi akiweka saini kweny mkataba wa amani wa Khartoum wakati wa sherehe jijini Bangui Februari 6, 2019.
Mmoja wa washiriki wa makundi ya waasi akiweka saini kweny mkataba wa amani wa Khartoum wakati wa sherehe jijini Bangui Februari 6, 2019. AFP Photos/Florent Vergnes
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 1

Mkataba wa amani, uliotiwa saini jijini Khartoum nchini Sudan kwa ajili ya amani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, unaonekana kutoheshimiwa kati ya serikali na waasi, huku pande zote zikilaumina.

Matangazo ya kibiashara

Makundi 5 kati ya 14 yenye ushawishi mkubwa ambayo yalisaini makubaliano ya amani na serikali ya Bangui hivi karibuni, yametoa muda wa saa 72 kwa rais wa Jamuhuri na waziri wake mkuu kurejelea upya uundwaji wa serikali mpya iliotangazwa Jumapili iliopita.

Makundi hayo ya waasi ambayo yanadaiwa kudhibiti asilimia 80 ya nchi, yamesema serikali iliotangazwa Jumapili haikuzingatia makubaliano ya amani ya huko Kharthoum, hivyo yametishia sio tu kujiondoa kwenye makubaliano lakini pia kuhakikisha kila mmoja anabeba jukumu lake.

Makundi hayo ya waasi yalitaraji kuona miongoni mwa wajumbe wa serikali ni kutoka makundi hayo, jambo ambalo serikali inasema nafasi ni ndogo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.