Pata taarifa kuu
DRC-CENCO-SIASA

Kambi ya Kabila na ile yaTshisekedi wakubaliana kuunda serikali ya muungano

Rais anayemaliza muda wake Joseph Kabila, kulia, na mrithi wake Félix Tshsiekedi wakati wa kuapishwa kwa rais mpya Kinshasa, Januari 24, 2019.
Rais anayemaliza muda wake Joseph Kabila, kulia, na mrithi wake Félix Tshsiekedi wakati wa kuapishwa kwa rais mpya Kinshasa, Januari 24, 2019. © REUTERS
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Washiriki wa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi pamoja na wale wa mtangulizi wake, Joseph Kabila, Jumatano wiki hii, wamekubaliana kuhusu uundwaji wa serikali ya muungano wa kitaifa.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inafungua njia kuelekea uteuzi wa mtu ambaye atakabidhiwa jukumu la kufanikisha upatikanaji wa Waziri Mkuu, Vyombo vya habari nchini DRC vimeripoti.

Katika hatua nyingine kiongozi wa Upinzani wa Lamuka Martin Fayulu, na Mkurugenzi mkuu wa ofisi ya rais Vital Kamerhe wamekataa kushiriki vikao vya Bunge.

Martin Fayulu anasema suala hilo haliingii akilini yeye kama rais aliyechaguliwa na wananchi haina maana yeye kuitwa mbunge, nchini humo.

Hata hivyo Kanisa Katoliki nchini DRC limeendelea kusema kuwa matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na Tume ya uchaguzi DRC (CENI) hayaendani na ukweli halisi wa matokeo ya uchaguzi.

CENCO inasema kulingana na ukweli wa matokeo ya uchaguzi, Martin Fayulu ndiye aliibuka mshindi wa uchaguzi wa urais wa DRC.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.