MALI-USALAMA

Mali: Kambi ya jeshi yashambuliwa, askari 21 wauawa Dioura

Kundi la wapiganaji wameshambulia kambi ya kijeshi ya Dioura, katikati mwa Mali (picha ya kumbukumbu).
Kundi la wapiganaji wameshambulia kambi ya kijeshi ya Dioura, katikati mwa Mali (picha ya kumbukumbu). AFP/Thomas Coex

Jeshi la Mali limepata pigo jingine tena siku ya Jumapili baada ya kambi yake katika jimbo la Dioura kushambuliwa na wapiganaji wa kijihadi ambapo taarifa ya jeshi la Mali inasema wanajeshi 21 wamepoteza maisha katika shambulio hilo.

Matangazo ya kibiashara

Wakaazi wa mji wa Dioura wameendelea kuwa na hofu baada ya kusikika kwa milio ya risase na zana nzito nzito wakati kambi ya jeshi katika eneo hilo ilipo shambuliwa ambapo hadi Jumapili mchana hakuna aliethubutu kwenda kambini.

Baadae jioni taarifa ya jeshi ilieleza kuwa shambulio lilitekelezwa na wapiganaji wa kijihadi wanaoongozwa na Ba Ag Moussa alieasi jeshi na kujiunga na wapiganaji wa kiongozi wa Kitwareg Iyad Ag Ghaly.

Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika, kabla ya shambulio hilo, kundi la wapiganaji wa kijihadi lilijipenyeza katika mji huo wa Dioura. Siku ya Jumamosi kundi jingine la wapiganaji wa kijihadi waliingia katika mji huo wakitumia pikipiki pamoja na magari ambapo kundi moja lilielekea kaskazini mwa kambi huku lingine kusini mashariki, ambapo milio ya risase ilisikia, magari ya kijeshi yaliteketezwa. Inadaiwa kuwa waasi hao waliondoka na silaha kadhaa za jeshi.

Kuhusu idadi ya waliopoteza maisha kumekuwa na mkanganyiko kuhusu ni wangapi waliopoteza maisha? Jeshi linasema wanajeshi 21 ndio waliouawa katika shambulio hilo dhidi ya kambi. Ni wangapi waliojeruhiwa, wangapi ambao hawajulikani walipo, na je kuliwa na waliotekwa? Bila shaka inahitaji subira ili kufahamu baadae kuhusu maswali hayo licha ya kwamba baadhi ya familia za wanajeshi zimeanza maombolezo.