DRC-USALAMA-SIASA

Mkutano muhimu kufanyika DRC, baada ya matokeo ya uchaguzi wa Maseneta

Wafuasi wa rais mpya Félix Tshisekedi, Kinshasa, Januari 24, 2019 (picha ya kumbukumbu).
Wafuasi wa rais mpya Félix Tshisekedi, Kinshasa, Januari 24, 2019 (picha ya kumbukumbu). © John WESSELS / AFP

Rais wa DRC Felix Tshisekedi anatarajiwa kukutana na wanasiasa wa chama chake UDPS na wale wanounga mkono muungano wa CACH unaongoza nchi hiyo, baada ya matokeo mabaya ya uchaguzi wa maseneta wiki iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Kama ilivyokuwa katika uchaguzi wa wabunge, muungano wa rais wa zamani Jospeh Kabila, imeibuka mshindi katika Uchaguzi huo huku chama cha UDPS kikishindwa kupata hata kimoja katika mkoa wa Mbuji Mayi, suala ambalo lilisababisha machafuko na polisi mmoja kupoteza maisha.

Mkurugenzi kwenye ofisi ya rais Felix Tshisekedi, Vital Kamerhe, ametangaza kwamba mkutano "muhimu" utafanyika Jumatatu, Machi 18, baina ya taasisi baada ya kutokea virugu katika miji kadhaa, kufuatia matokeo ya uchaguzi wa maseneta . Pia ametangaza kwamba baada ya mkutano huo "hatua muhimu" zitatangazwa.

Jumamosi, wafuasi wengi wa chama cha UDPS waliandamana katika miji kadhaa kupinga wabunge wao ambao wanawashtumu kwamba walikula rushwa kwa kuwachagua maseneta kutoka muungano unaomuunga mkono Joseph Kabila wa FCC, ambao umepata wingi wa viti katika bunge la Seneti.