MSUMBIJI-ZIMBABWE-MAJANGA YA ASILI

Kimbunga Idai: Mvua zatatiza shughuli za uokoaji Msumbiji

Raia wanajaribu kutafuta maji katika kijiji cha Praia Nova nchini Msumbiji.
Raia wanajaribu kutafuta maji katika kijiji cha Praia Nova nchini Msumbiji. ©Josh Estey/Care International via REUTERS

Kulingana na ripoti ya hivi karibuni, Kimbunga Idai kimeua watu zaidi ya 100 nchini Zimbabwe na zaidi ya 200 nchini Msumbiji, nchi iliyoathirika zaidi. Katika mji wa Beira, mji ulioathirika zaidi, bado kuna watu ambao wamekwama juu ya paa za nyumba na ambao wanahitaji kuokolewa.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo, maelfu ya watu wamekwama na wanahitaji msaada wa kuondolewa katika baadhi ya maeneo yanayokumbwa na mafuriko kwa sasa. Mashirika ya kihisani na watu wanaojitolea wanaendelea na shughuli ya uokoaji, licha ya kuwa hali bado ni tetekutokana na ukumbwa wa janga hilo.

Maelfu ya watu hawana msaada wowote, na ni vigumu kufika katika maeneo waliko kutokana na mafuriko yanayokumba mkoa huo.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya maswala ya kibinadamu imeonya kwamba kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, "hali hiyo inaweza kuwa mbaya zaidi."

Alberto Mondlane, gavana wa mkoa wa Sofala amethibitisha kutokea kwa hali mbaya kama hakutakuwa na msaada wowote wakati mvua zikiendelea kunyesha. "Mafuriko yanaendelea wakati kuna watu wengi ambao wamekimbilia juu ya miti au juu ya paa zanyumba. Wanasubiri msaada, " amesema gavana Alberto Mondlane.

Shughuli za uokozi na hata ugavi wa misaada kusaidia mamia ya maelfu ya waathirika wa kimbunga hicho zinatatizwa kutokana na uharibifu wa barabara lakini pia mawasiliano yaliokatika kutokana na kimbunga hicho.

Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa mataifa wanachama kujitokeza kufadhili operesheni ya misaada baada ya kimbuka hicho kiloichotokea siku sita zilizopita kilichopiga mataifa ya Msumbiji, Zimbabwe na Malawi.

Shirika la Medecin Sans Frontieres ambalo linatoa misaada katika maeneo yalioathirika limesema hali bado ni tete kama anavyoeleza hapa Marie Christine Ferir.